- BUWSSA itatumia njia muafaka za mawasiliano kuwahabarisha wateja wake juu ya katizo la huduma lililopangwa kwa kuzingatia mambo yafuatayo:
- Muda ambao katizo limepangwa kutokea.
- Maeneo yatakayoathirika.
- Sababu za katizo la huduma ya Maji.
- Matarajio ya Muda ambao huduma itarejeshwa.
- Taarifa itatolewa kabla ya siku 3 ya katizo lililopangwa mfano linalohusu usafishaji wa chemba za maji.
- Kwa wateja wakubwa, BUWSSA na wateja watakubaliana juu ya mpango wa katizo. Kama haitawezekana, BUWSSA itatuma taarifa kwa watumiaji wakubwa wa huduma ya Majisafi, kwa maandishi (barua halisi), Simu au kupitia Barua pepe.
- Kwa katizo la Maji ambalo halikupangwa na ambalo litaathiri sehemu kubwa (ikiwemo kuzimika kwa gridi ya Taifa) BUWSSA itaujulisha umma/wateja binafsi sababu za katizo. BUWSSA itachagua njia muafaka ya mawasiliano kuwajulisha wateja wake kuhusiana na katizo lolote la umeme ndani ya saa 24.
- Kwa katizo la umeme lisilopangwa kwa mteja mmoja mmoja au maeneo madogo, BUWSSA itafanya bidii ya kurudisha maji ndani ya saa 24 kutegemeana na aina ya tatizo baada ya umeme kurudishwa.
- Kwa tatizo ambalo haliwezi kurekebishwa ndani ya kipindi hicho kama vile kuharibika kwa mitambo mikubwa kutokana na matatizo ya kiufundi, wateja watajulishwa muda wa kurejesha huduma baada ya matengenezo kukamilika. Hata hivyo kwa matatizo madogo BUWSSA itarudisha maji ndani ya saa 12.