Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bunda (BUWSSA) inaendeshwa na Bodi ya Wakurugenzi wapatao 8 ambao huteuliwa kuwakilisha vikundi au makundi ya watu katika jamii ya watumiaji maji wa Mji wa Bunda kulingana na umuhimu wa kila kundi.
1. MUUNDO WA BODI YA WAKURUGENZI
- Mwenyekiti wa bodi.
- Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji.
- Mkurugenzi Mtendaji wa BUWSSA
- Mwakilishi wa Madiwani.
- Mwakilishi wa kundi la Watumiaji wakubwa.
- Mwakilishi wa kundi la Wafanya Biashara.
- Mwakilishi wa kundi la Watumiaji maji Majumbani.
- Mwakilishi kutoka Wizara ya Maji.
2. MAJUKUMU MAKUU YA BODI
- Kusimamia na kutathimini shughuli zote za Mamlaka.
- Kupitisha mipango ya kazi na Bajeti.
- Kiungo kati ya Wizara na Mamlaka.
- Kuajiri na kuachisha kazi watumishi.
- Kuwawakilisha wateja na kusikiliza malalamiko yao pamoja na wadau.
- Kusikiliza maoni ya watumishi na kutoa ushauri.