WhatsApp Image 2024-01-15 at 15.51.57
Nyabehu Mradi (2)
BODI
KIKAO CHA BODI YA WAKURUGENZI YA BUNDA WSSA
previous arrowprevious arrow
next arrownext arrow

Mhe. Joshua Mirumbe
Mwenyekiti wa Bodi

Bi. Esther Gilyoma
Mkurugenzi Mtendaji

 

DIRA NA DHIMA

DIRA

Kuhakikisha kuwa inakuwa Mamlaka ya mfano kwa kutoa huduma bora zaidi Tanzania.

 

DHIMA

“Kutoa huduma ya majisafi, salama na ya kutosha katika mazingira rafiki yanayoridhisha  wateja.

Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira Bunda (BUWSSA) ipo katika mji wa Bunda ambao upo km 156 toka Jiji la Mwanza. Mji huu upo kando kando ya Barabara itokayo Mwanza kwenda Musoma,  na Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira Bunda ilianzishwa kwa sheria namba 8 ya mwaka 1997 iliyofanyiwa marekebisho katika sheria Na.12 ya mwaka 2009 ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Na sheria Na.12 ya mwaka 2009 iliyofanyiwa marekebisho katika sheria Na. 5 ya mwaka 2019.

Mamlaka ya Maji Bunda ilitangazwa kwenye  gazeti la serikali no.235 la tarehe 10/7/2009. Pamoja na Mamlaka nyingine 28 zikiwemo kwa Sheria Na. 12 ya mwaka 2009 iliyoanza kutumika rasmi 1/8/2009.

Mamlaka hii ni ya daraja “B”. Hii ikimaanisha kuwa Mamlaka ina wajibu wa kugharamia gharama zote za uendeshaji na matengenezo.

Madhumuni ya kuundwa kwa Mamlaka za Maji ni kutoa huduma endelevu ya usambazaji wa maji kwa kuzingatia dhana ya uendeshaji shughuli kibiashara.

Mamlaka inafanya kazi chini ya Bodi ya Wakurugenzi na kwa mujibu wa Mkataba wa Maridhiano (MoU) baina ya Mamlaka na Wizara inayohusika na Maji na pia inafanya kazi chini ya udhibiti wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (“EWURA”).

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bunda ni Mamlaka inayojitegemea  iliyoanzishwa na Sheria tajwa hapo juu na katika kufanya kazi zake Mamlaka inaongozwa na dira, dhima na kanuni.

"FUNGUA MAJI BOMBANI, UPATE UHAI, KAZI IENDELEE"

MATANGAZO

HUDUMA ZETU

Huduma zitolewazo na mamlaka ya maji Bunda ni kama zifuatazo;

    1. Kutoa huduma ya majisafi na salama
    2. Kutoa huduma ya usafi wa mazingira hasa ( maji taka)

JINSI YA KULIPA

  1. Kupitia Benki: Fika tawi lolote au Wakala wa benki ya NMB, CRDB na Namba ya kumbukumbu ya malipo.
  1. Kupitia Mitandao ya Simu:
        • Ingia kwenye menu ya mtandao husika
        • Chagua 4 (Lipa Bili)
        • Chagua 5 (Malipo ya Serikali)
        • Ingiza Namba ya kumbukumbu ya malipo (Iliyopo kwenye bili)
        • Ingiza kiasi cha pesa
        • Weka namba ya siri