Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira Bunda (BUWSSA) ipo katika mji wa Bunda ambao upo km 156 toka Jiji la Mwanza. Mji huu upo kando kando ya Barabara itokayo Mwanza kwenda Musoma, na Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira Bunda ilianzishwa kwa sheria namba 8 ya mwaka 1997 iliyofanyiwa marekebisho katika sheria Na.12 ya mwaka 2009 ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Na sheria Na.12 ya mwaka 2009 iliyofanyiwa marekebisho katika sheria Na. 5 ya mwaka 2019.
Mamlaka ya Maji Bunda ilitangazwa kwenye gazeti la serikali no.235 la tarehe 10/7/2009. Pamoja na Mamlaka nyingine 28 zikiwemo kwa Sheria Na. 12 ya mwaka 2009 iliyoanza kutumika rasmi 1/8/2009.
Mamlaka hii ni ya daraja “B”. Hii ikimaanisha kuwa Mamlaka ina wajibu wa kugharamia gharama zote za uendeshaji na matengenezo.
Madhumuni ya kuundwa kwa Mamlaka za Maji ni kutoa huduma endelevu ya usambazaji wa maji kwa kuzingatia dhana ya uendeshaji shughuli kibiashara.
Mamlaka inafanya kazi chini ya Bodi ya Wakurugenzi na kwa mujibu wa Mkataba wa Maridhiano (MoU) baina ya Mamlaka na Wizara inayohusika na Maji na pia inafanya kazi chini ya udhibiti wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (“EWURA”).
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bunda ni Mamlaka inayojitegemea iliyoanzishwa na Sheria tajwa hapo juu na katika kufanya kazi zake Mamlaka inaongozwa na dira, dhima na kanuni.
DIRA
“Kuhakikisha kuwa inakuwa Mamlaka ya mfano kwa kutoa huduma bora zaidi Tanzania.“
DHIMA
“Kutoa huduma ya majisafi, salama na ya kutosha katika mazingira rafiki yanayoridhisha wateja.“
MALENGO YETU
- Kuboresha upatikanaji wa MajiSafi na Salama.
- Kuboresha makusanyo ya mwezi ya huduma ya Majisafi.
- Kuboresha makusanyo ya mwezi ya huduma ya Majitaka.
- Kuboresha utunzwaji wa Mazingira na Uhifadhi wa vyanzo vya maji.
- Kufanikisha kuboresha na kuongezwa kwa sheria ya MajiSafi na Usafi wa mazingira.
MISINGI YETU
Katika kutekeleza majukumu yetu tumejipangia kuwa na misingi ya utekelezaji wa majukumu yetu kama ifuatavyo;-
- Kutimiza Dira na Dhima ya Mamlaka.
- Wateja Kwanza
- Watumishi ni Rasilimali namba moja ya Mamlaka
- Wafanyakazi kuhimizwa kujifunza na kubadilishana maarifa
- Uwazi
- Ukweli
- Uwajibikaji.
- Kuboresha na Kukuza Ushirikiano na Kujituma
- Kuwajibika kwa jamii inayotuzunguka