MAELEZO YA JINSI YA KULIPIA BILL (MAELEZO KWA MTEJA)
- KWA NJIA YA SIMU ZA KIGANJANI
- Malipo yanaweza kufanyika kupitia huduma za simu za kiganjani (TIGOPESA, M-PESA, AIRTELMONEY, T-PESA, HALOPESA, EZYPESA) kwa kupitia mitandao mbalimbali ya simu kama ifuatavyo;
- Ingia kwenye menu ya mtandao husika
- Chagua 4 (Lipa Bili)
- Chagua 5 (Malipo ya Serikali)
- Ingiza Namba ya kumbukumbu ya malipo (Iliyopo kwenye bili)
- Ingiza kiasi cha pesa
- Weka namba ya siri
Namna ya kulipia kwa Tigopesa
- Piga *150*01#
- Chagua namba (4) “Lipa Bili”
- Chagua (5) “Malipo ya Serikali”
- Ingiza namba ya kumbukumbu ya malipo (Control number)
- Ingiza kiasi cha pesa unachotaka kulipa
- Ingiza namba ya siri kuhakiki
Namna ya kulipia kwa M-Pesa
- Piga *150*00#
- Chagua namba (4) “Lipa kwa M-Pesa”
- Chagua (5) “Malipo ya Serikali”
- Chagua namba 1 Namba ya Malipo
- Ingiza namba ya kumbukumbu ya malipo (Control Number)
- Ingiza kiasi cha pesa unachotaka kulipa
- Ingiza namba ya siri
- Thibitisha kwa kuchagua (1)
Namna ya kulipia kwa airtelmoney
- Piga *150*60#
- Chagua namba (5) “Lipia Bili”
- Chagua (5) “Malipo ya Serikali”
- Chagua namba 1 “Weka namba ya kumbukumbu”
- Ingiza namba ya kumbukumbu ya malipo (control number)
- Ingiza kiasi cha pesa
- Weka namba ya siri
Namna ya kulipia kwa T-Pesa
- Piga *150*71#
- Chagua namba (5) “Lipia Bili”
- Chagua (3) “Malipo ya Serikali”
- Ingiza kumbukumbu namba (control number)
- Ingiza kiasi
- Ingiza namba ya siri
Namna ya kulipia kwa halopesa
- Piga *150*88#
- Chagua namba (5) lipia bili
- Chagua (5) malipo ya serikali
- Weka namba ya kumbukumbu ya malipo (control number)
- Ingiza kiasi cha pesa
- Weka namba ya siri
Namna ya kulipia kwa Ezypesa
- Piga *150*02#
- Chagua namba (8) malipo ya serikali
- Chagua (1) Tanzania Bara
- Weka namba ya kumbukumbu ya malipo (control number)
- Ingiza kiasi cha pesa
- Weka namba ya siri
- KWA NJIA YA KUWEKA FEDHA BENKI (DIRECT BANK DEPOSIT)
Malipo yanaweza kufanyika kwa kuweka fedha katika benki zifuatazo, mfano: NMB, CRDB kwa kupitia matawi ya benki, mawakala wa Benki na njia nyingine za malipo zitolewazo na Benki. Tumia Namba ya kumbukumbu ya Malipo (Control Number) uliyopewa unapofanya Malipo.
- KWA NJIA YA KUHAMISHA FEDHA (TISS)
Malipo yanaweza kufanyika kwa njia ya kuhamisha Fedha kutoka benki moja kwenda benki nyingine ndani ya Tanzania (TISS). Mteja / Mlipaji atapatiwa fomu za kuhamishia fedha na Mamlaka ya Maji Bunda baada ya kuichapisha (Printed Transfer Form / Bill) na ataipeleka na kuiwasilisha katika benki atakayoitumia kuhamisha fedha na hatatakiwa kujaza upya fomu.