MAUNGANISHO MAPYA YA HUDUMA YA MAJI

  1. Wateja wapya ambao hawajajiunga na huduma ya maji wanakaribishwa sana kujiunga na huduma hii muhimu.
  2. Unapohitaji huduma ya maji, tafadhali fika ofisini kwa ajili ya kupata maelezo sahihi ya kitaalamu na ushauri sahihi wa hatua za kuchukua ili uweze kupata huduma ya maji safi nyumbani kwako, kiwandani kwako. nk. 
  3. Fomu zinapatikana Ofisi ya Huduma kwa Mteja bila malipo yoyote na Mteja atalazimika kuja na picha 2 ndogo za rangi (passport) pamoja na nakala ya kitambulisho cha Mpiga kura au NIDA au Uraia au Leseni ya udereva au Barua toka serikali ya mtaa au barua kutoka taasisi zinazotambulika.
  4. Gharama za uunganishaji wa huduma ya maji zinatofautiana kati ya mteja  mmoja na mwengine hivyo  usiogope kujiunga kwa kuhofia gharama.
  5. Tahadhali, unapo pata maelekezo kwa mtu asiye husika anaweza akakushauri vibaya na unaweza ukaingia kwenye matatizo au hasara kama atakushauri kukiuka taratibu au sheria ya maji.

Baada ya kupewa makadirio ya gharama, mteja anatakiwa kulipa gharama za kuunganisha maji ndani ya siku 30. Gharama zitabadilika/kuongezeka iwapo mteja atalipia baada ya siku 30 kupita ili kufidia ongezeko la bei za bidhaa endapo litatokea.

  1. BUWSSA inaruhusu malipo ya maunganisho ya maji kwa fedha itakayolipwa kwa mkupuo mmoja kupitia Benki / wakala wa benki na mitandao ya simu.
  2. Mteja ataunganishiwa maji ndani ya siku 7 baada ya kukamilisha utaratibu wa malipo wa Mamlaka.
  • Malipo yote yanatakiwa yafanyike kupitia benki (CRDB au NMB) na mitandao ya simu kwa kutumia Control Namba (kumbukumbu namba ya malipo) kisha mteja kuleta risiti ya malipo Ofisini kwa ajili ya uhakiki.

NB:

  • Mamlaka haitahusika na mapatano au malipo yoyote yatakayofanywa nje ya utaratibu uliowekwa na Mamlaka.
  • Maunganisho yasiyo halali kwenye miundombinu ya maji ya Mamlaka na wizi wa maji ni kosa la jinai na adhabu yake kwa anayepatikana na hatia ni faini au kifungo au vyote viwili kwa pamoja kama ilivyo kwenye sheria ya maji na usafi wa Mazingira Na.5 ya mwaka 2019.