MAJUKUMU YA MAMLAKA
i) Kuhakikisha kuwa huduma ya maji inawafikia wateja wetu wakati wote, katika wingi na ubora wa viwango vinavyotambulika Tanzania.
ii) Kupendekeza kwa Bodi ya Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira – Mji wa Bunda (BUWSSA), viwango vya gharama za kulipia huduma ya maji vitakavyowezesha kukidhi mahitaji ya kugharimia uendeshaji na matengenezo utakaowezesha upatikanaji wa majisafi na salama kwa uhakika bila kuathiri au kupendelea sehemu yoyote ya jamii.
iii) Kukuza na kupanua mfumo wa usambazaji maji utakaofikisha huduma hiyo kwenye maeneo yote ya mji wa Bunda na vijiji vinavyouzunguka.
iv) Kuibua, Kupanga, kusimamia na kutekeleza miradi mipya ya majisafi na salama kwa mfano miradi ya Nyabehu – Bunda, Migungani – Kaswaka na mtandao wa usambazaji wa 32KM, Ujenzi wa chujio, pamoja na kuweka mtandao mpya wa maji Mjini Bunda.
v) Kushirikisha, Kuelimisha na kufahamisha watumiaji wa maji juu ya matumizi bora ya maji, uhifadhi wa vyanzo vya maji na masuala yote yanayohusu maji.Kushirikiana na Wizara inayosimamia sekta ya maji, Ngazi ya Mkoa, Wilaya, na wadau wengine katika uandaaji na utekelezaji wa mipango yenye kulenga katika upanuzi endelevu wa huduma ya maji na kukusanya mapato kutoka kwa wateja wake.
vi) Kuhifadhi mazingira katika eneo lote la kiutendaji la Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira – Mji wa Bunda (BUWSSA) lililotambuliwa kwa mujibu wa sheria ili kuhakikisha kuwa hakuna uharibifu wala uchafuzi wa mazingira pamoja na kuibua mipango endelevu ya utunzaji wa mazingira.
vii) Kuwashirikisha wadau kwa kuitisha semina mbalimbali zenye lengo la kuelimisha wananchi juu ya huduma ya maji pamoja na shughuli za Mamlaka
viii) Kuheshimu wajibu na kutekeleza majukumu yote kama ilivyoainishwa kwenye mkataba wa makubaliano kati ya Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira – Mji wa Bunda (BUWSSA), Halmashauri ya Mji wa Bunda na Wizara ya Maji; aidha, kuzingatia viwango vya ubora katika utekelezaji kulingana na makubaliano na EWURA.
ix) Kutoa taarifa kwa viongozi wa Wizara ya Maji, Mkoa na Halmashauri ya Mji wa Bunda juu ya matukio yote makubwa ambayo yanaathiri au yanaweza kuathiri utoaji wa huduma bora ya maji mjini Bunda
x) Kuandaa na kuwasilisha taarifa za kila mwezi, nusu mwaka na mwaka mzima Wizara ya Maji kwa wakati.
xi) Kuandaa Bajeti ya kila mwaka na kuiwasilisha Wizara ya Maji baada ya kuidhinishwa na Bodi ya Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira – Mji wa Bunda (BUWSSA).