KUSITISHIWA HUDUMA YA MAJI KWA MTEJA
- Mamlaka itamuondolea huduma mteja atakayeshindwa kulipa ankara ya mwezi baada ya siku 30 tangu alipopata Ankara ya maji.
- Wateja wanaweza wasipewe taarifa nyingine ya ziada zaidi ya iliyoko kwenye Ankara ya madai ambayo ni notisi iliyojitosheleza kabla ya kusitishiwa huduma.
- Kusitishwa kwa huduma kutafanyika wakati wowote endapo mteja atagundulika kuwa anatumia maji kinyume na sheria na kwa njia isivyo halali. Hatua hii itaenda sambamba na kuchukuliwa hatua za kisheria.
- Wateja waliowahi kuondolewa kwenye huduma na kukutwa wamejirudishia huduma isivyo halali wataondolewa tena kwenye huduma na kuchukuliwa hatua za kisheria.
- Mamlaka haitamuondolea mteja huduma siku zifuatazo;
UREJESHWAJI WA HUDUMA
- Mteja atakayesitishiwa huduma ya maji kwa kutolipia ankara atarejeshewa huduma baada ya kulipa deni analodaiwa na adhabu ya kutolipa deni husika kwa wakati ndani ya masaa 24.
- Wateja watakao ondolewa huduma kutokana na kujiunganishia huduma ya maji bila halali watarejeshewa huduma baada ya kulipa ada husika, fidia ya maji waliyotumia na adhabu.
- Baada ya kukubaliana na Mamlaka kuhusu namna ya kulipa deni.
- Baada ya kubaini kwa uhakika kwamba mteja aliondolewa huduma kimakosa.
- Kama uondoaji huo ulitokana na shughuli za kiutendaji na kiufundi za Mamlaka.