Wafahamu Watumishi Vinara wa BUWSSA

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bunda (BUWSSA) imeweka utaratibu wa kupima utendaji kazi wa Watumishi wake ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa BUWSSA Bi. Esther Gilyoma ametangaza dau nono zaidi kwa Watumishi wanaofanya kazi vizuri katika vitengo vyao ili kuchochea Watumishi kutoa huduma bora kwa wananchi wa Bunda kwa kujituma usiku na mchana na kufikia malengo waliyojiwekea katika vitengo vyao kwa tija ya Mamlaka.

Mkurugenzi Gilyoma hutoa Hati za Pongezi na Motisha ya fedha kwa watumishi wanaofanya vizuri kwa upande wa Makusanyo ya ankara za maji (Kitengo cha Huduma kwa Wateja), Ufundi hodari na Usukumaji wa Maji (kitengo cha Usambazaji Maji na Usimamizi wa Usafi) na Utawala (inajumuisha Kitengo cha Rasilimali watu na Utawala, Kitengo cha TEHAMA na Takwimu, Kitengo cha Ukaguzi wa ndani, Kitengo cha Fedha na Uhasibu, Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi na Kitengo cha Huduma za Sheria).

Hadi sasa Mtumishi Naomi Jonathan kutoka Kitengo cha Huduma kwa Wateja ameweka rekodi ya kuibuka kinara mara 3 mfululizo katika ukusanyaji wa Ankara za maji.

ORODHA YA VINARA KWA KILA  MWEZI NI KAMA IFUATAVYO

MWEZIMKUSANYAJI BORAFUNDI HODARIMSUKUMA MAJI BORAUTAWALA
MACHI 2025Reuben Mwijarubi (Bunda Stoo A)                  –
FEBRUARI 2025Martha Phinias (Ukerewe Road)Eng. Hamdan Msalu (Mhandisi II – Uendeshaji na Matengenezo)Sunday Ijengo (Migungani)  Josephine Hizza (Afisa Manunuzi II)
JANUARI 2025Naomi Jonathan (Kabarimu)Khamis Mgeta (Balili)Maria George (Ushashi)Ahazi Damson (Mwandishi Mwendesha Ofisi II)
DISEMBA 2024Naomi Jonathan (Kabarimu)Elias Masanyiwa (Nyasura)Akoth Ngito (Mugaja)
NOVEMBA 2024Naomi Jonathan (Kabarimu)Estomi Elieza (Kabarimu)Maganga Paulo (Migungani)
OKTOBA 2024Paschal Patrick (Balili)Kasanda James (Kabarimu)Iddy Zubery Said (Nyabehu)
SEPTEMBA 2024Delvin Denis (Manyamanyama)
AGOSTI 2024Emmanuel Boniphace (Nyasura)

Kinara wa Mwezi Machi 2025

Vinara wa Mwezi Februari 2025

Vinara wa Mwezi Januari 2025

Vinara wa Mwezi Disemba 2024

Vinara wa Mwezi Novemba 2024

Vinara wa Mwezi Oktoba 2024

Vinara wa Mwezi Septemba 2024

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*