
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bunda (BUWSSA) inawataarifu wateja wake kuwa kutakuwa na ukosefu wa huduma ya maji kwa siku ya Jumatano tarehe 03/09/2025 na Alhamisi tarehe 04/09/2025 (kwa siku mbili).
Sababu: Kuruhusu matengenezo ya bomba la 16″ lililopasuka maeneo ya Tairo na Bunda Stoo.
Matengenezo hayo yataathiri upatikanaji wa huduma ya majikwa wakazi wa Mji wa Bunda, huduma ya upatikanaji wa maji itarejea mara baada ya matengenezo hayo kukamilika.
BUWSSA, inaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.
Leave a Reply