Mnamo tarehe 23/04/2025, Mkutano Mkuu wa Wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bunda (BUWSSA) umemchagua Mtumishi Estomi Elieza kutoka Idara ya Usambazaji Maji na Usimamizi wa Usafi kuwa Mfanyakazi Hodari wa BUWSSA kwa mwaka 2025.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, Bwn. Abdulrahmani Kombo ambaye ni Meneja Rasilimaliwatu na Utawala wa BUWSSA amemtangaza Bwn. Estomi kuibuka kidedea kwa kupata kura 21 kati ya 34 zilizopigwa. Bwn. Kombo aliwapongeza na kuwashukuru watumishi wote waliohudhuria kwa kufanya uchaguzi wa haki na uliozingatia vigezo.
Kwa upande wake, Mfanyakazi Hodari aliyechaguliwa, Bwn. Estomi Elieza amewashukuru Watumishi wote kwa kumuamini na kuridhishwa na utendaji wake na kuahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na ushirikiano mkubwa.
BUWSSA, Kazi Iendelee.!!!

Leave a Reply